SHAIRI: SISI NA WAO

Standard

Related image

Kuna sisi, na wao wasio nasi

Sisi ni sisi na wao mafisi

Sisi kwa sisi, kwa zetu nafsi

Wao, si kwa sisi, wao kwa zao nafsi.

 

Sisi ni sisi.

Wao, walikuwa sisi

Waliishi na sisi

Walikula na sisi

Walilala na sisi

Walizaliwa na sisi

Walikuwa sisi.

 

Sasa, wao ni wao

Wala vyao

Wana vyao

Walala kwao

Waoana wao

Wapendana wao

Wao kwa wao.

 

Sisi, tuliwatoa wao

Sio ili wawe wao

Ili wawe wao kati ya sisi

Wachache wao wengi sisi

Ili wao watusaidie sisi

 

Tukawapa vyetu sisi

Wakalala petu sisi

Walaka vyetu sisi

Wakatukalia sisi

Wakatufanya wajinga sisi

Wakatufanya watumwa sisi.

 

Wakubwa wao

Miungu wao

Wafalme wao

Matajiri wao

Wamenawiri wao.

 

Masikini sisi

Malofa sisi

Wapuuzi sisi

Walala hoi sisi

Wa matopeni sisi

Waswahili sisi

Makapuku sisi

 

Wametunyonya sisi

Wametupora sisi

Wametuibia sisi

Wametutupa sisi

Wametupumbaza sisi

Wametupofua sisi

Wametupa uziwi sisi

 

Tumewachoka sisi!

Wachache kuliko sisi

Wengi sisi

Tusimame sote sisi

Tutuchukue chetu sisi

Tuwe tena sisi!

 

© Mwl. Paul Mndima ’17

Limetungwa Wednesday, May 3, 2017  KuhaririwaSunday, May 7, 2017 11:20:10 PM

Limetolewa Monday, July 24, 2017 

PIcha na: gopsy.ru

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s