PANZI NA KUNGURU

Standard

PANZI NA KUNGURU

art.jpg

Panzi, alikuwapo panzi. Na jamii yake.
Kunguru, alikuwapo kunguru. Na jamii yake.

Panzi na jamii yake walijua kujificha,
Kunguru na jamii yake njaa kutwa kucha.

Kunguru na jamii yake walinoa makucha,
Panzi na jamii yake kuwafanya mabucha.

Basi jamii yake, ikamtuma kunguru,
Kwenda kwa Panzi na jamii yake kuomba udhuru,

Kunguru, na jamii yake wakaomba uchumba,
Panzi, na jamii yake wakampokea mchumba.

Kunguru, na jamii yake wakaandaa karamu,
Panzi na jamii yake wakahudhuria kwa hamu

Panzi na jamii yake wakashiba hakika,
Kunguru, na jamii yake wakafurahi hakika

Mwisho ukafika, sherehe kuhitimika,
Kunguru kamshika, panzi kampika.

Jamii ya kunguru nayo kufaidika.
Jamii ya panzi yote kuifyeka.

Funzo, adui ajaye kwa upanga, ni bora kuliko ajaye mikono nyuma.

Wakikuuliza ni nani kasema haya, waambie ni mwalimu Paul Mndima

Wednesday, April 5, 2017 7:22:30 AM

Advertisements

4 thoughts on “PANZI NA KUNGURU

  1. Musnad

    Ni funzo zuri sana,nimependa lakini pia miye ni mshairi natunga na kughani pia na napenda kusoma na kuskiliza kazi za washairi wengine na ndo maana nikaipenda na hii

    Liked by 1 person

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s