SHAIRI: NAFSI YANGU

Standard

 

logo.png

 

Nafsi yangu:

Nafsi yangu nakupenda, Sinae mwingine ni wewe tu.

Nafsi yangu nakujali. Nitafanya liwalo uridhike tu.

Nafsi yangu nakuthamini. Nitafanya yote nikulinde tu.

Nafsi yangu nakuthamini. Nitafanya kila juhudi nisikupoteze tu.

Nafsi yangu nakuheshimu. Nitafanya yote uyatakayo ufurahike tu.

Nafsi yangu, nakupenda. Ntafanya yote. Usiniponze tu.

 

Ulitamani maini, na wali wa biriani, nikaenda sokoni nipate kukufariji mwandani.

Nikanunua na jabari, mwenye afya na mnono,

Nikakupikia na futari, ukaridhika kwa uhondo.

Ukasema wataka na sharubati, ya mapera na matikiti,

Nikafanya shuruti, ufurahie, nakutumikie mie wako kiti.

 

Ukashiba, ukatulia, na bilauri ya maji nikakupatia.

Ukaukumbuka mtemba, na shisha ukaitaka,

Nikaufanya mtemba na shisha nikaikoka,

Tukaketi kwa mkeka tukisema twafurahika.

 

Jioni kufika, ukataka na komoni,

Kwa kata na birika, tukajinywea bandani,

Ofa washikaji faidika, tukijitamba kilabuni

Hata macho nikarembua, nikirudi nyumbani.

 

Usiku ukafika, minofu ya samaki,

Na sima ya mihogo, kwa mboga sukuma wiki.

Kula kwa bi mdogo, maji moto kukandwa kwa ustadi,

Usingizi ukaja kwa unono, baada ya kuikamilisha ya ndoa jadi.

Kitanda swafi maridadi, na blanketi kwa baridi.

 

Nafsi yangu, nimefanya, japo sio yote, nimejitahidi

Nafsi yangu, nimesema, japo sio yote, nimejitahidi

Nafsi yangu, nimekupa, japo sio yote, nimejitahidi

Nafsi yangu, nimekulisha, japo sio vyote, nimejitahidi

Nafsi yangu, nimefikia mwisho, sasa wanataka nini?

 

Unapenda magari kwa mamia,

Unataka wanawake kwa kila tabia,

Unaniomba niongeze na masuria,

Unaniambia wanne hatatoshi kutulia.

 

Unataka papa kwa sinia, sahani ati haitatoshea,

Ubwabwa mchele kwa gunia, ati kibaba kinywani chaishia,

Kutembea nchi za dunia, na matamasha ya kila tasnia,

Watumwa na wafenyikazi kwa mamia na kasri la kujivunia.

 

Unataka pombe za ghaibuni, komoni mbege za nini,

Za kunukia sabuni, ya makumbi maliwato hupendi tundu chini

Marashi na uturi, ubani na udi ya ghali manukato

Wakati mie sifuri, sina kitu nikununulie yale yote utakayo

 

Nafsi yangu, umekuwa fisi, mwezi kwenye maji na haujui kuogelea,

Nafsi yangu, umekuwa paka, upeo uwezo mdogo kila kitu kujua,

Nafsi yangu, umekuwa njiwa, kuukimbilia mtama juu ya ulimbo kutua,

Nafsi yangu umekuwa mbwa, mkono ukulishao haufai kuuma

 

Nafsi yangu, sasa tuko gizani, eti sasa angalau ugali na bamia unalilia.

Aaaah nafsi yangu.

 

(c) Paul Mndima 2016

 

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s